Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Shirikisho la Soka la Palestina limetangaza kuwa siku ya Jumatano, Suleiman Obeid maarufu kama Pele wa Palestina, aliuwawa kishahidi karibu na mstari wa kusubiri msaada wa kiraia, wakati utawala wa Kizayuni wanywa damu ulipofanya mauaji hapo.
Mchezaji huyu wa miaka 41 alipata jina la Pele wa Palestina kutokana na historia yake bora ya michezo, na katika historia ya mechi zake na timu ya taifa ya Palestina alikuwa amefunga mabao 100.
Baada ya tukio hili, UEFA katika ukurasa wake wa X iliandika: “Kwaheri kwa Suleiman Obeid, Pele wa Palestina” na kuonesha nafasi yake kama kielelezo kwa vijana wa Palestina, huku ikiwa haujataja chochote kuhusu sababu ya kifo chake au namna alivyouwawa, Kwa masikitiko, UEFA inaficha kila kitu kuhusiana na suala hili.
Ukimya huu ulimfanya Salah kutoa radi amali ya moja kwa moja kwa kusema: “Je, mnaweza kusema aliuawa vipi na wapi!?”
Kabla ya hapo, Salah pia alikuwa ametoa misaada mingi kwa taasisi za kibinadamu zinazounga mkono Palestina.
Chanzo: BBC
Maoni yako